Tuesday, September 30, 2014

RAIS wa Afghanistan asaini mkataba na NATO


Rais Ashraf Ghani

SIKU  moja baada ya kuapishwa kwa rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani, serikali yake imetia saini mkataba mpya wa usalama na shirika la kujihami la NATO.

Mkataba huo utaidhinisha zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili, wengi wakiwa wamarekani, kusalia nchini Afghanistan hata baada ya kumalizika kwa kandarasi yao mwaka huu.
Mkataba huo ulitiwa sahihi katika hafula iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni na mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa wa Afghanistan Hanif Atmar na balozi wa Marekani nchini humo Jim Cunningham, huku Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani akishuhudia.

No comments:

Post a Comment