MFANYAKAZI wa
Umoja wa Mataifa aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia katika hospitali moja
nchini Ujerumani.
Madaktari katika hospitali ya Leipzig
wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne
asubuhi.
Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu
mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na
Nigeria.
No comments:
Post a Comment