Timu ya Tiafa ya Tanzania |
TIMU ya Taifa
ya Tanzania, "Taifa Stars" imeibuka na ushindi mnono dhidi ya Benin
baada ya kuicharaza magoli 4-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio
katika kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, FIFA.
Kabla ya mchezo uliopigwa katika
dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania ilikuwa
ikishika nafasi ya 115 katika viwango vya ubora vya Fifa duniani, ikishika
nafasi ya 34 barani Afrika, huku Benin ikiwa katika nafasi ya 78 duniani na 18
barani Afrika.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na
Nadir Haroub Cannavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu na Juma Luizio akiifungia
timu yake magoli mawili, huku la kufutia machozi la Benin likitumbukizwa wavuni
dakika ya 90 ya mchezo na Ssegnon Stephane anayechezea timu ya West Bromwich
Albion ya England.
Katika uwanja huo huo wa Taifa kabla
ya mchezo wa Tanzania na Benin, mchezo mwingine wa kuvutia ulizikutanisha timu
za viongozi wa dini waliochanganyika katika timu mbili wakiwemo Mashekhe na
Maaskofu.
Viongozi hao waliunda timu za Amani
na Mshikamano, ambapo Amani waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mchezo huo ulilenga kuonyesha
ushirikiano wa kijamii kati ya waumini wa dini kubwa mbili nchini Tanzania za
Waislam na Wakristo.
No comments:
Post a Comment