Tuesday, October 14, 2014

FIFA yatakiwa kuwa wazi katika uendeshaji wa shughuli zake


Rais  wa FIFA Sept Blater

MCHUNGUZI  mkuu wa maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA, amesema shirikisho hilo linapaswa kuonyesha uwazi kuhusu linavyoendesha shughuli zake.

Mchunguzi huyo ambaye pia ni wakili mjini New York, Michael Garcia, ameandika ripoti kuhusu uchunguzi unaohusiana na madai ya ufisadi katika mchakato wa kura ya nchi itakayoandaa michuano ya kombe ya dunia mwaka 2018 na 2022.
Lakini FIFA haiko tayari kuchapisha ripoti hiyo kuambatana na masharti na sheria zake kuhusu siri za shirikisho hilo.
Michael Garcia anataka FIFA kubadilisha mfumo unaotumiwa kuendesha shughuli zake hasa kuhusiana na maswala yenye usiri mkubwa.

No comments:

Post a Comment