Thursday, October 16, 2014

TASO Morogoro yapata viongozi wapya


Viongozi wa TASO wakikagua vipando nanenane Morogoro

CHAMA cha Wakulima TASO kanda ya Mashariki TASO kimepata safu mpya ya uongozi utakaoongozwa na Mwenyekiti mpya Sallim Mwaking’inda utakaodumu madarakani kwa miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. 


Uongozi huo tayari umekabidhiwa ofisi mbele ya Mwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo Oktoba 15 katika ofisi ya TASO kanda ya Mashariki zilizo ndani ya uwanja wa maonesho ya wakulima Nanenane 'uwanja wa Mwl. Julius K.Nyerere' nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Waliochaguliwa kukiendesha chama hicho katika kipindi hicho nyadhifa zao kwenye mabano ni pamoja na
mwanamke pekee katika safu hiyo Zahara Kitima(Makamu mwenyekiti ),Ndumayi Mukama(Katibu Mtendaji) na Amanzi  Amanzi(Mwekahazina ).

Baada ya makabidhiano kwa nyakati tofauti Mwenyekiti mpya wa TASO Mwaking’inda na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Swalehe Yangeyange walisisitiza kupanua wigo wa umuhimu wa maonesho hayo kwa kushirikisha uongozi uliopita na wadau wa sekita mbalimbali za maendeleo nchini hususani Kilomo ili maonesho hayo yawe na tija kwa mkulima na jamii.


Hata hivyo Mwakinginda alianza kazi kwa kusitisha ajira za wafanyakazi wote wa  TASO ofisini hapo hadi vikao vya kamati tendaji vitakapo kaa na kuwajadili upya utumishi wao kama unafaa au laa.

Baadhi ya makabidhiano katika ofisi hiyo,Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Yangeyange alikabidhi  funguo,hati ya umiliki uwanja sambamba na nyaraka mbalimbali za kiofisi.
Awali Mwenyekiti wa Taso Taifa Engelbert Moyo aliutaka  uongozi mpya kuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato sambamba na kuongeza vivutio vya uwanja ili utumike kwa kipindi chote cha mwaka katika maonyesho na kuongeza tija kwa umma.

No comments:

Post a Comment