Katibu mkuu wa Nishati na madini Eliakimu Maswi |
KATIBU
mkuu Wizara ya madini na nishati
Eliakim Maswi amewatoa hofu yakutofukuzwa au kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi wa
shirika la Tanesco kutokana na serikali kuanzisha mkakati na mwelekeo wa
kurekebisha mapungufu mbalimbali katika mfumo wa utumishi katika wizara hiyo.
Akifungua kamati ya kubadilisha
sekta ndogo ya umeme nchini wenye lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma za umeme,kuimarisha hali ya kifedha ya TANESCO,kuvutia wawekezaji wadogo,kupunguza
ruzuku ya serikali kwa Tanesco katibu huyo alisema mpango huo unalenga
kumpunguzia mzigo mlaji wa umeme.
“Ili kutekeleza mpango huu ni lazima
kuwe na rasilimali watu na fedha za kutosha...hatuna wazo wala mpango wa
kupunguza wafanyakazi na hata kiwango cha Mega watts zinazozalishwa"Maswi
aliwatoa hofu wafanyakazi.
Alisema mbali na hilo serikali
inakuja na mpango wa kuwahakikishia usalama wa ajira kwa kuboresha elimu
zao makazini,stahili na mikataba yao ikiwa ni kufikia tija iliyokusudiwa
kupitia sekta hiyo.
Awali Mwenyekiti kamati ya maendeleo
Tanesco Abdul Mkama aliiomba serikali kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo kuondoa hofu na mashaka juu ya maslahi na ajira yao pia
siasa zianzoenea mitaani kuwa shirika linavunjwa na kuundwa upya jambo ambalo
limekuwa likiwaathiri.
“Tunaomba dira ya mageuzi isipite
ili iwe faida kwa wafanyakazi tunaomba dira maalum na si mabadiliko toka kwa
viongozozi tofauti na magari mawili kwa ajili ya wafanyakazi” alisisitiza
Mkama.
Baadhi ya wafanyakazi akiwemo Msoma
mita Ramadhani Butallah alitaja baadhi ya kero wanazokutana nazo kuwa ni
ongezeko la mita mbovu ambazo zimekuwa zikisoma taarifa tofauti na matumizi
hivyo kuamsha hasira za wateja dhiidi yao.
“wafanyakazi waelimishwe juu ya madhara
ya kutoa bili isiyo sahihi,vishoka wanaolitia hasara shirika wadhibitiwe kwa
kuchukuliwa hatua kali za kisheria lakini pia serikali iweke ukaguzi wa mara
kwa mara kwenye mita za umeme ” alisema Butallah.
Wakati serikali inakusudia
kupandisha idadi ya wateja kutoka asilimia 24 hadi kufikia 50 ya watanzania
wote inakusudia kuanzisha soko huru la nishati ya umeme lenye ushindani.
No comments:
Post a Comment