Katibu mkuuwa ccm Abdulrahman Kinana |
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) kimeonyesha hofu ya jimbo la kilombero
kuchuliwa na upinzani kutokana na chama hicho kutafunwa na 'kansa' ya ubinafsi
kwa wanachama wake.
"kumbukeni tayri hapa Kilombero tumepoteza kata Tano ikiwemo ya Utengule, Mchombe,Lumemo,Ifakara na Kidatu...hii manayake nini jimbo linakwenda hili nyie chezeni tu"aliwasihi kwa tahadhari.
Hayo yalisemwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa Kanali mstaafu Harun Kondo wakati akihitimisha ziara yake katika kata za wilaya ya Kilombero kuelimisha na kutoa mwongozo wa chaguzi zijazo.
Katika ufafanuzi wake Kondo alisema kuna wanachama ambao
kazi yao ni kuangalia maslahi binafsi badala ya chama na wanachi jambo ambaalo
ni kansa inyotakiwa kukingwa mapema kwa kutowapokea watu hao.
Aliwataka
wanachama hao kubadilika kwa kuondoa tofauti zilizopo wakiangalia walipojikwaa
na kujenga mshikamano wenye dhamiria ya kuukabili upinzani katika chaguzi
zijazo.
Aidha alikitaka chama kuwa na tathimini nzuri za wagombea kukubalika akibainisha kumekuwa na tabia chama hicho kusimamisha wagombea wasiokubalika jambo linalokikigharimu fedha nyingi na mbinu nyingi kufanikisha ushindi.

No comments:
Post a Comment