Wednesday, October 8, 2014

GUNINITA aitaka serikali na wakulima wa miwa kuunusuru zao hilo


Mkulima wa miwa akiwa shambani

MKULIMA wa Miwa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani Dar es salaam John Guninita ameibuka na utabiri kuwa zao hilo litakufa miaka miwili ijayo endapo serikali na wakulima nchini hawatakutana haraka na kuunda ajenda ya kulinusuru.


Akizungumza mjini Ifakara,mkoani  Morogoro,Guninita ambaye ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa katika bonde la Kilombero alisema zao hilo tegemeo kubwa kwa wananchi na uchumi wilayani humo litakufa kutokana na thamani ya miwa kushuka mwaka hadi mwaka .

"mfano msimu uliopita wakulima tumeuza hadi shilingi 55,000 kutoka shilingi 67,000 kwa tani...sasa upo uwezekano mkubwa tukakimbilia kulima Mpunga"alifafanua

Amebainisha kuwa msingi mkubwa wa tatizo hilo la kushuka kwa bei ni watu binafsi kupitia mikono ya serikali kuagiza sukari nyingi toka nje ya nchi na ongezeko kubwa la njia za panya mipakani.

Aidha aliongeza kuwa sera ya kumlinda mlaji inachangamoto kubwa katika uboreshaji pato la mkulima wa miwa nchini kwakua sukari ya nje imekuwa ikilipiku soko la sukari ya ndani kutokana na tofauti kubwa ya bei ya bidhaa hizo.

"nadhani jukumu la kuagiza sukari nje ya nchi lipewe wenye viwanda ili wadhibiti kikamilifu uchakachuaji na kuongeza tija kwa mkulima wa nadani badala ya mfumo wa sasa kwani unawaumiza wakulima hasa wadogo"aliongeza.
Hata hivyo alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kutoa mikopo yenye mashariti rahisi,kukuza mitaji ya wakulima kwa kuingiza vyombo vingi vya mikopo kwani linaelekea kumuinua mkulima kiuchumi.





No comments:

Post a Comment