Wednesday, October 8, 2014

WAFANYAKAZI wilaya ya Chemba huenda wakagoma kulipa michango ya mwenge


Watumishi wa wilaya ya Chemba , mkoani Dodoma

WAFANYAKAZI wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba mkoni Dodoma wanakusudia kugoma kufanya kazi baada ya serikali wilayani humo kuzuia mishahara yao kwa miezi mitatu sasa kwa madai ya kutochangia shilingi 50,000 za mbio za Mwenge.


Uamuzi wa wafanyaka kazi hao wakiwemo wa idara nyeti ya Afya,Elimu,Kilimo na Maji katika halmashauri hiyo kugoma unakuja kutokana na mateso ya kufungiwa mishara yao halali Benki hadi watakapo lipa fedha hizo.

Wakizungumza mwishoni mwa wiki kwa sharti la kutotajwa majina yao kuhofia utumishi wao,badhi yao walisema uongozi wa wilaya hiyo ukiongozwa na mkuu wa Francis Mtinga na Mkurugenzi Dk.Willium Mafwere umekuwa ukitumia mabavu kuwanyanyasa katika hakizao katika mabo yasiyowahusu.

Wakithibitisha unyanyasaji wanaofanyiwa na viongozi hao wafanyakazi hao walionyesha barua kumbu namba CDC/A,60,3VOL1,76  ya tarehe 14/7/2014 kicha cha habari 'malipo ya sherehe za mwenge' iliyosainiwa na Mselem Aziz kwa niaba ya Mkurugezi.

Katika barua hiyo uongozi huo ulitoa tahadhari kwa wafanyakazi hao kulipa fedha hizo haraka kabla ya 20/7/2014 vinginevyo mishara yao itasimamishwa hadi hapo watakapo lipa deni jambo linatekelezwa tangu mwezi Julai mpaka sasa.

Walipotafutwa kutoa ufafanuzi wa madai hayo mkurugenzi na mkuu wa wilaya walipisha katika kauli zao wakati Dk Mafwere anadai hakuna kitu kama hicho kwake Mkuu wa wilaya Mtinga alikili kuwepo zoezi hilo kwa lengo la kulipa deni la fundi nguo.

"sikiliza bwana usiniulize upuuzi huo kwangu hakuna kitu kama hicho...kwanza wewe nani hadi uulize mambo kama hayo! Alihoji Dk.Mafwere na kudai naingia kanisani kusali.

Katika majibu yake mkuu wa wilaya alisema uamuzi wa kuzuia mishahara ya watumishi hao inatokana na watumishi hao kutokuwa na ubinadamu dhiidi ya fundi aliyechukua jukumu la kuwashonea suti nzuri kwa bei hiyo bila kulipwa ujira wake

No comments:

Post a Comment