Wednesday, October 8, 2014

WHO;EBOLA kuenea barani Ulaya


Zsuzsanna Jakab, Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya

SHIRIKA  la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuwa kuenea kwa virusi vya ebola barani Ulaya ni jambo ambalo kwa kiasi kikubwa haliweza kuepukika.

Zsuzsanna Jakab, Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya ametoa taarifa hiyo Jumanne hii, masaa machache baada ya kesi ya kwanza ya maambukizo ya homa ya ebola kuthibitishwa huko Uhispania.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani barani Ulaya ameongeza kuwa maambukizo ya ebola yatatokea katika siku za usoni kwa kuzingatia safari nyingi zilizopo kutoka nchi za Ulaya kuelekea nchi zilizoathirika na mlipuko wa homa hiyo.
Jakab amesema kuwa wafanyakazi wa sekta ya afya katika nchi za Ulaya wako katika hatari kubwa, hata hivyo akasema kuwa jambo lenye umuhimu mkubwa kwa mtazamo wao ni kwamba, bara la Ulaya bado lipo katika kiwango cha hatari ndogo na kwamba eneo la magharibi la bara hilo limejiandaa vyema kukabiliana na homa nyingine za maambukizi ikiwemo ebola.  


No comments:

Post a Comment