Thursday, October 9, 2014

FIFA: Uingereza yatafunwa na ubaguzi wa rangi


Jeffrey Webb

MKUU  wa kitengo cha kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika shirikisho la soka duniani FIFA amesema kuwa ubaguzi wa rangi katika soka ya Uingereza unafanyika hadharani.

Jeffrey Webb amesema kuwa ubaguzi unafanywa wazi na kuangazia ukosefu wa watu weusi na wale waliotengwa katika mikutano.
Afisa mkuu wa muungano wa wachezaji wa kulipwa Gordon Taylor ametaja ubaguzi wa rangi kama tatizo lililofichwa.
lakini Webb amesema kuwa swala hilo halijafichika bali halizungumziwi katika mikutano.
Web ambaye pia ni naibu rais wa FIFA pamoja na mkuu wa shirikisho la soka katika mataifa ya Carribean ,kazkazini na katikati mwa Marekani alimtumia mkufunzi wa vijana katika kilabu ya Chelsea Eddie Newton kama mfano wa tatizo hilo.


No comments:

Post a Comment