Saturday, October 11, 2014

WANANCHI wa Mindu wako hatarini kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu


Add caption

WANANCHI wa kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro wako  hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na matumbo kwa kutumia maji ya vidimbwi na makorongoni licha ya kukabidhiwa mradi mkubwa wa maji  na Benki ya dunia wa visima virefu uliogharimu zaidi ya shilingi Mil.250.



Mradi huo ambao tayari umekabidhiwa na mbio za mwenge mwaka huu tayari umekufa na mkandarasi kutoweka licha ya kutakiwa kuwepo eneo la mradi kwa uangalizi kwa miezi 18 huku zaidi ya shilingi Mil.5 zilichangwa na wanachi kuunga mkono mradi huo zikiyeyukia benki katika mazingira ya kutatanisha.

Baadhi ya wanachi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti akiwemo Rehema Hussen na mwenyekiti wa mtaa wa Lugala Willison Mizola walisema kufa kwa mradi huo kunatokana na udhaifu wa serikali pitia halmashauri ya manspaa hiyo katika kusimamia.

Kwa upande wake mwenyekitia Mizola ,mbali na kukili kuwepo kwa mradi huo bubu alisema tangu maji yatoke siku ulipofunguliwa nambio za Mwenge maji yanatoka mara moja kila baada ya wiki mbili na kuwalazimu wanachi kutumia maji ya vidimbwe na makorongoni.
Alitaja baadhi ya shuguli zilizoekelezwa na mkandarasi ili kuzifikia zaidi ya kaya 13,000 kuwa ni pamoja na kuchimba visima,kufunga mashine za kuvuta na kusambaza maji mitaani,kujenga vituo 13 vya kuchota maji vyenye umbali wa mita 100 kutoka kituo kimoja hadi kingine.
Alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa jambo hilo,Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jolvis  Simbeye hakupatikana hata hivyo Diwani wa kata hiyo Hamis Msasa alikili kusuasua kwa upatikanji maji katani humo kwa madai kuwa wanachi wanashindwa kumudu gharama za jenereta ya kuvuta na kusambaza maji.
Aliongeza kuwa kutokana na gharama ya uendeshaji kuonekana kuwa kubwa,kata wamekubaliana kuurejesha mradi huo chini ya mamlaka ya majisafi na mazingira MORUWASA ili ushugulikiwe huko badala ya sasa unavyoendeshwa  na Manspaa.



No comments:

Post a Comment