Walemavu wakiwa katika ofisi yao Ilala Bungoni |
JUMUIYA ya
Uchumi na maendeleo ya walemavu nchini (JUMAWATA)itaadhimisha siku ya
kumbukumbu ya kifo cha Mwl Julius Neyrere inayofanyika kila tarehe 14,
oktoba kwa kufany a usafi wa mazingira katika eneo lao la mradi
lililopo Mtamba wilayani Kisarawe, mkoawa Pwani.
Akiongea na Mbiu
ya Maendeleo katika ofisi ya Jumawato iliyopo Ilala Bungoni , Manispaa ya Ilala
,jijini Dar es salaam hivi karibuni, Katibu wa JUMAWATA Bwana John Abeid amesema kuwa , wameamua kufanya hivyo, lengo likiwa ni kufanya
tathmini ya mradi huo wa ujenzi wa makazi ya walemavu na shule ya jumuiya hiyo ulioanza mwaka 2008.
Katibu huyo
amrzitaka Taasisi, Jumuiya, makampuni na
watu binafsi kujitokeza kwa wingi siku ya oktoba 14, ili kujumuika na walemavu
ikiwa ni pamoja na kuchangia fedha na
vitu katika kufanikisha shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment