Thursday, October 23, 2014
MAWAZIRI wa zamani wa Raisi Karzai kufikishwa mahakamani kwa ufisadi
MAWAZIRI watano wa serikali ya Hamid Karzai rais wa zamani wa Aghanistan watafunguliwa mashtaka mahakamani, kwa tuhuma za kufanya ufisadi na ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma.
Basir Azizi Msemaji wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Afghanistan amesema kuwa, Mir Muhammad Amin Farhang aliyekuwa Waziri wa Biashara, Inayatullah Qasemi na Hamidullah Qaderi waliokuwa Mawaziri wa Uchukuzi, Mir Muhammad Siddiq Ishan aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Madini na Muhammad Jalil Shams aliyekuwa Waziri wa Uchumi ni miongoni mwa shakhsia ambao wanatuhumiwa kufanya ufisadi mkubwa kwa kutumia nyadhifa zao.
Hatua hiyo imechukuliwa katika hali ambayo, miaka minne iliyopita Mwendesha Mashtaka wa serikali ya Kabul aliwahi kutoa tuhuma kama hizo dhidi ya maafisa 20 wa ngazi za juu serikalini, lakini hakuna kesi yoyote iliyowahi kusikilizwa mahakamani hadi leo hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment