Thursday, October 9, 2014
TAMASHA la kupinga uharamia wawanyama pori kufanyika Morogoro
MTANDAO wa Habari za kijamii nchini wenye makao yake makuu mkoani Morogoro(MHAKITA) unatarajia kufanya Tamasha kubwa la michezo kupiga vita uharamia na ukatili dhidi ya wanyamapori wakiwemo Tembo,Twiga na Faru ambao wanaelekea kuisha katika hifadhi za nchini.
Sambamba na hilo pia kuhamasisha jamii hususani iliyo jirani ha hifadhi za wanyama na misitu nchini kuimarisha ulinzi kwa faida ya uchumi wa Taifa na jamii kwa jumla.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtandao huo Merina Robert alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa alisema tamasha hilo linalotaraji kuzinduliwa Oktoba 12 tarafani Mikumi nila siku saba.
"Tamasha hili tumeliandaa kwa ushirikiano na Hifadhi ya Taifa (TANAPA),kwa kuanzia vijiji saba kati ya vijiji ishirini vinavyozunguka hifadhi ya Taifa Mikumi kikiwemo cha Doma,Ruhembe,Kitete,Kielezo, Mkata,Mikumi na Lumango vitahusika moja kwa moja"alisema Merina.
Alisema tamasha hilo lenye kauli mbiu 'Ddumisha michezo piga vita ujangili' litakwenda sambamba na maonyesho ya vitendo vya ukatili na uharamia dhiidi ya wanyama pori na misitu katika baadhi ya hifadhi nchini.
Aidha aliofafanua kuwa kutakuwa elimu juu ya kuheshimu mipaka ya hifadhi ikijikita zaidi kuwaelimisha wanachi juu ya umuhimu na faida za kuhifadhi maliasili hususani katika kipindi hiki chenye mabadiriko makubwa hali ya hewa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment