Thursday, October 9, 2014

TGNP yandaa semina kuhusu uchaguzi wa viongozi kwa makundi maalum



WATU wa Mkundi malumu katika jamii mkoni Pwani wamekutana mjini hapa kujadili mbinu za za kupata viongozi waadilifu na njia kupata njia zitakazo wawezesha kushinda chaguzi za uongozi serikalini unaotaraji kuanza Desemba kwa serikali za mitaa na kuhitimishwa mwakani kwa kupata viongozi wa serikali kuu.


Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mtandao wa jinsia nchini TGNP,viongozi na makundi maalumu waliokutanishwa ni pamoja Wanawake,walemavu,vijana,viongozi wa dini na asasi mbalimbali mkoani humo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mradi huo Gloria Shechambo wahusika wote waliokutanishwa hapo wanatoka katika wilaya tatu ikiwemo ya Kibaha ,Kisarawe na Bagamoyo .

Gloria alisema mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha wadau wa maendeleo kujenga ushawishi na kuongeza ufahamu katika kupata viongozi wenye ari ya kupinga uyanyasaji na mawazo mgando yanayosababisha Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kutengwa  hususani katika chaguzi.

Wakizungumzia mafunzo hayo baadhi ya washiriki akiwemo Jane Omary  na Khalfan Ismail walisema mafunzo hayo yamekuja katika kiopindi ambacho jamii inauhitaji mkubwa wa ufahamu kuhusu mbinu na jinsi ya kukabiliana na changamoto za uchaguzi.





No comments:

Post a Comment