Wednesday, October 1, 2014

WATU mia moja wafariki kutokana na njaa



SHIRIKA moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu linasema kuwa zaidi ya watu mia moja wamefariki kutokana na njaa pamoja na maradhi katika kambi moja ya kijeshi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Shirika hilo Human Rights Watch, limesema kuwa watu hao ambao walikuwa wapiganaji wa zamani na wake zao pamoja na watoto walihamishwa katika kambi nyingine iliyotengwa Kaskazini mwa DRC.
Ilikuwa baada ya wao kujisalimisha kutoka kwa kundi la wapiganaji Mashariki ya nchi.
Walipokea chakula kidogo na huduma ya afya baadhi wakiponea kifo kwa kuiba chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima.












No comments:

Post a Comment