Wednesday, November 5, 2014

KONGOZI wa CUF Morogoro mjini ajiunga na CCM


Mwenyekiti wa CUF taifa Prof Ibrahimu Lipumba

KATIKA hali isiyo ya kawaida tukielekea kwenye uchaguzi wa
 serikali zamitaa Desemba 24,mwenyekiti kwa misimu miwili
 Mtaa wa Konga kata ya Kingo kupitia chama cha wanachi CUF
 Hamis Simba amebwaga manyanga na kuahamia chama cha
 mapindizi CCM.


 Simba ambae kwa uamuzi wake huo amefanyiwa tafrija ndogo na
chama hicho cha CCM kata ya Sabasaba ikiongozwa na mwenyekiti
 wake Fikiri Juma alisema ameamua kufanya hivyo baada ya
 kuchoshwa na siasa zisizo na manufaa kwake na familia yake.


 Alisema kwa muda mrefu amekuwa akiipima CCM na vyama vingine
 na kubaini kuwa ccm ndio chama pekee kinachojali wananchi
 wake hata sera zake zinatekelezeka kikamilifu na hakina
 marumbano kama vilivyo vyama vingine vya siasa nchini
 kikiwemo cha CUF.

 Mara baada ya kumpokea na kumkabidhi kadi mpya,mwenyekiti wa
 ccm Manspaa ya morogoro Fikiri Juma alisema hizi ni salamu
 ya mvua za rasharasha kwa vyama vya upinzani kuwa 2015
 wataangukia pua.

No comments:

Post a Comment