Wednesday, November 5, 2014

WAKULIMA wa mbogamboga Kilosa waomba kusaidia mbinu za kuongeza thamani mazao


Wakulima wa mbogamboga Kilosa, Morogoro

WAKULIMA wa mbogamboga na viungo wilayani Kilosa wameiomba
 serikali,taasisi,makampuni na watu binafsi nchini kote
 kujitokeza kuwekeza katika kuongeza thamani,ufungaji bora na
 kuyawezesha mazao hayo kudumu kwa muda mrefu ili wanufaike
 nayo.


 Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ziara ya mafunzo
 iliyoandaliwa na Halmashauri hiyo na mashirika ya kiraia
 ikiwemo Mviwata,Ibrahim Mlima na Nasibu Hussen walisema
 wanaomba viwanda hivyo ili wanufaike na kilimo hicho ambacho
 kwa sasa kimefikia zaidi ya asilimia 50 ya wanachozalisha
 kuharibikia shamba.

 Walisema ziara hiyo iliyowakutanisha wakulima wa kijiji cha
 Kibunga ,Ulaya na Mbuyuni wilayani humo katika bustani za
 kijiji cha Ibingu imewafumbua macho baada ya kubaini kuwa
 mazao mengi ya wazalishaji nchini yanaharibikia shamba kwa
 kukosa viwanda kama hivyo.

Awali afisa kilimo kutoka mtandao wa wakulima wadogo nchini
Mviwata Amanzi Amanzi aliwataka wasomi nchini kuanza kuni
 njia zitakazofanikisha kutegua changamoto ya upotevu wa
 mazao mashambani ili yawanufaishe wakulima amabao wengi wao
 huishia kubaki na madeni baada ya kuzalisha.

 Aidha aliwataka maafisa ugani kutekeleza kwa vitendo kazi na
 fani waliyosomea kwa kuwa karibu na wakulima  hususani
 katika kipindi hiki cha kuelekea utayarishaji wa mashamba
 hadi kuvuna ili wazalishe kwa tija.


No comments:

Post a Comment