CHUO Kikuu cha kilimo cha Sokoine cha Morogoro |
MRADI wa tafiti bunifu za kilimo (AGRI)
unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani (USAID) ikishirikiana na chuo
kikuu cha Sokine cha kilimo (SUA) na wizara ya kilimo chakula na Ushirika
umeanza safari ya kuzalisha wasomi wataalamu wabunifu 135 nchini watakao
kabiliana na changamoto za kilimo kupitia bunifu zao katika sekta hiyo na
lishe.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa
Mradi huo kutoka Marekani Profesa David Kraybill na Msaidizi wake kutoka SUA
Profesa Issac Minde walipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za MOROPC
mjini hapa.
Katika
Mradi unalenga kuzalisha wataalamu
katika ubunifu huo kati yao nusu wakiwa wanawake, kufanya tafiti za kisayansi
katika bara la Afrika,Amerika ya kasikazini na Asia,kukifanya SUA kuwa chuo cha
usalama wa chakula nchini na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania,Mrekani na
nyingine katika katika masuala hayo.
“vyuo vikuu vya marekani kikiwemo
cha Michigan, Ohio,Virginia Tec,Tuskegee,Florida na chuo kikuu cha lowa Stete
tayri vimezalisha wasomi 67 wakiwemo 51 wa sahahada ya uzamili,16 shahada ya
uzamivu”alisema
Katika fafanuzi zake aliongeza kuwa
wanachuo 30 vyuo vya Afrika kikiwemo
SUA-Tanzania,Makerere-Uganda,Lilongwe-Malawi,Nairobi,Kenyatta,Jomo
Kinyata,Egerton vya Kenya,Stellenbosch cha Afrika ya kusini na chuo kikuu cha
Zambia”Aliongeza
Profesa Kraybill alisema mbali na
vyo hivyo wanafunzi 35 wakiwemo 10 wa shahada ya kwanza na wawili sahada ya
uzamimivu walihitimu mafunzo yao chuo kikuu cha SUA na wanafunzi sita wako chuo
kikuu cha Punjab nchini India.
Kwa upande wake Profesa Minde mbali
na kupongeza mafanikioa makubwa tafiti zilizo zalishwa,iAGRI pia imekiwezesha
chuo kuimarisha njia za ufunshaji,kusaidia upatikanaji tafiti,SUA kuwa na
mahusiano mazuri na yenye tija kwa chuo,mhitimu na jamii.
No comments:
Post a Comment