Waislamu wakiwa katika siku ya ASHURA |
MAMILIONI ya Waislamu kote duniani wanashiriki katika
hafla za maombolezo ya Siku ya Ashura, ambayo hufanyika kwa mnasaba wa
kukumbuka kuuawa shahidi Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS pamoja
na wafuasi wake huko Karbala.
Mamilioni ya
waombolezaji katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi zingine duniani
wamejitokeza mitaani, misikitini na kumbi za kidini maarufu kama Husseiniya kwa
ajili ya kukumbuka Siku ya Ashura, ambayo ni siku ya 10 ya Mwezi Mtukufu wa
Muharram.
Waumini kote
Iran wamesimamisha sala ya jamaa wakati wa adhuhuri kukumbuka namna Imam
Hussein AS pamoja na mashahidi wengine wa Karbala walivyosimamisha sala ya
jamaa kwa wakati pamoja na kuwa katika hali ngumu ya vita.
No comments:
Post a Comment