MJI wa St
Louis limeshuhudia maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha
uamuzi wa kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.
Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta
madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.
Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar
amesema alisikia milio ya risasi takriban 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9
Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani
walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.
No comments:
Post a Comment