Tuesday, November 25, 2014

VIJANA Kilombero wapatiwa mafunzo ya ufyatuaji tofari



VIJANA 40 wilayani Kilombero wameanza mafunzo ya siku saba kufyatua tofari za kisasa,gharama nafuu na rahisi katika ujenzi wa nyumba na kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira pia kuondosha tatizo laajira na kuinua kipato kwa vijana.


Mratibu na msimamizi wa mafunzo hayo yanyotolewa na shirika la nyumba nchini NHC  Castol Malulika alisema lengo la mpango huo ni kuharakisha maendeleo kwa kuboresha ujenzi wa makazi bora kwa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Malulika NHC ambayo imetoa mashine nne kwa vijana na mafunzo hayo pia shilingi laki tano zinataraji kutolewa kwa kila kikundi kitakachoanzishwa kwa kazi hiyo kama ruzuku ya mtaji.
Baadhi ya vikundi vilivyoanza kunufaika na mafunzo hayo kwa mujibu wa mratibu huo ni pamoja na Mtandao Mbasa toka kata ya Kibaoni,Ujenzi Lumemo toka kata ya Lumemo,Vijana Mlabani na Vijana Wandewa vyote kutoka kata ya Ifakara.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala ameishukuru NHC kwa kubuni mpango huo kwani utaongeza ajira kwa vijana na ujenzi wa nyumba bora zenye gharama nafuu na wao kama wilaya watazidi kuwahimiza na kuwahamasisha vijana wengi kuingia katika shughuli hii.

Amewaagiza vijana kuwa elimu watakayopata ni vema wakaitumia ipasavyo katika ujebzi wa nyumba bora na kuamini nyumba bora na zenye gharama nafuu zitapatikana wilayani humo.
Aidha Masala amewakumbushia vijana hao kuwa katika vikundi wajaribu kuwa na viongozi imara wenye uwezo wa kuongoza,upendo na wenzao wenye kujitoa na kuchochea maendeleo yao na ambao wanaheshimu na kufuata kanuni na taratibu walizojiwekea.



No comments:

Post a Comment