Tuesday, November 25, 2014

PROF Luhanga atabiri machafuko kutokana na tatizo la ajira


Jengo la chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar

UONGOZI wa chuo cha Biashara CBE nchini umetabiri mlipuko wa ugaidi na machafuko makubwa kwa Taifa kutokana na ongezeko la asilimia 8.8 la vijana na wasomi wasiokuwa ajira endapo serikali haitaandaa fursa za kundi hilo kujitegemea na kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwemo ya ujasilimali.


Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho wakati akimkaribisha Naibu waziri wa Viwanda na Biashara nchini Janeth Mmbene kuhudulisha wahitimu 1,797 kwenye mahafali ya 47 katika fani mabalimbali chuoni hapo kampasi ya Dodoma.

Profesa Luhanga alisema ikiwemo changamoto hiyo ya ukosefu wa ajira kwa vijana,pia kunachangamoto ya ongezeko kwa kasi wimbi la vijana linalokuwa kwa asilimia 8.8 na muindombunu duni ya kufundishia na kujifunzia hasa kuwandaa vijana kuhitimu elimu yenye tija kwao.

Alitoa wito kwa serikali kufanya utafiti wa kina utakao kuja na mapendekezo mbadala ya kuondosha tatizo hilo na kushauria zaidi vijana kuelimishwa ujasilaiamali na serikali kuunga mkono kwa kuziwezesha bunifu za wanachuo na wahitimu.

“sense ya 2012 inaonyesha kati ya takribani watu Mil.48 nchini asilimia 44 ni kundi la vijana waliochini ya maiaka 15 na vijana walio kati ya miaka 15-36 ni asilimia 36 wanaounda asilimia 84 ya vijana walio na umri kati ya miaka 0-36”alifafanua.

Kuhusu kukabiliana na changamoto hizo Profesa Luhanga alisema chuo kimenunua Hekta 39.2 eneo la Nzuguni manispaa hiyo ya Dododmana kuanza tafiti kujua wahitimu wake wako wapi kiutumishi na mchango wao kwa taifa ili kiboreshe mitaala yake kutokana na changamoto hizo hatari kwa taifa.



No comments:

Post a Comment