Thursday, November 6, 2014

OBAMA na Rebuplican waahidi kumaliza mvutano wa kisiasa


Rais wa Marekani Barack Obama

KIONGOZI  mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani.

Wanachama wa Republican wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani.

Kiongozi wa baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema ataliwezesha baraza hilo kufanya kazi na kupitisha miswada ya sheria.

No comments:

Post a Comment