Wauguzi wakiwa kazini |
KUNDI la wafanyakazi wa afya nchini Mali leo wanapewa chanjo ya
majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Hii ina maana kwamba watu
waliojitolea kufanyiwa chanjo ya majaribio nchini Mali kufikia watu 40.
Utafiti ulianza Mali kufuatia
majaribio salama kufanyika nchini Uingereza na Marekani.
Chanjo hiyo imetengenezwa na wanasayansi katika
Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza huko Maryland, nchini
Marekani na inatengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline
No comments:
Post a Comment