Thursday, December 25, 2014

JESHI la Burundi lawaonya wapinzania kutofanya maandamano

JESHI na Polisi ya Burundi zimewatahadharisha wapinzani wa nchi hiyo kufanya maandamano. 

Mkuu wa Vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Burundi sambamba na kuwataka wapinzani watupilie azma yao ya kuandamana.

Amesema kwamba nchi hiyo sio kama Burkina Faso. Meja Jenerali Prime Niyongabo amesisitiza kuwa, askari jeshi na vikosi vya usalama vitakabiliana vilivyo na watu ambao wanawashawishi wengine kuandamana.
Wapinzani wa Burundi wanaituhumu Tume ya Uchaguzi kuwa inapendelea chama tawala. Katika radiamali yao kwa ripoti ya Tume ya Uchaguzi kuhusu uandikishaji wapiga kura, wapinzani wametaka wajumbe wa tume hiyo wajiuzuru na kubatilishwa mchakato mzima wa uandikishaji majina ya wapiga kura wakidai kuwa udanganyifu mkubwa ulifanywa na chama tawala katika daftari la wapiga kura.
Duru za nchi hiyo zinaarifu kuwa asilimia 88 ya Warundi waliotimiza masharti ya kupiga kura wamejiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka ujao.


No comments:

Post a Comment