Thursday, December 25, 2014

NYILAWILA kuzichapa na Mmalawi mwakani

Bondia Nyilawila kulia akiwana bondia Said Mbelwa
BONDIA  wa Tanzania Karama Nyilawila mapema mwakani 2015 ,anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka malawi Frank Mwamaso katika pambano la raundi nane la uzani wa supermiddle litakalofanyika jijini Dar es salaam.

Nyilawila bondia namba mbili kwa ubora katika uzani wa supermiddle tayari ameisha saini mkataba amesema yupo tayari kupanda ulingoni kwa lengo la kuongeza kiwango cha ubora na mpaka sasa yupo katika mwanzo wa maandalizi kuweza kufanya vizuri katika pambano hilo.
Pambano hilo litasimamiwa na kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania( TPBC) chini ya kiongozi wake Chaurembo Palasa.



No comments:

Post a Comment