Kivuko Mto Kilombero, mkoani Morogoro |
KATIKA kipindi
cha miezi 11 mwaka huu kivuko cha mto Kilombero kimedaiwa kukusanya shilingi
776,229,336 katika makusanyo yake wakati wa uvushaji watu na magari.
Hayo yalisemwa na mkuu wa kivuko cha mto Kilombero Mhandisi Fadhil
HarounMeneja kwa niaba ya Meneja wa Temesa mkoa wa Morogoro Mhandisi Magreth
Mapula kwenye kikao cha bodi ya kivuko hicho kinachotoa huduma ya kuvusha watu
na vyombo vya usafiri viendavyo na kurudi wilayani Ulanga.
"katika kipindi cha Januari hadi Juni kivuko kilikusanya
shilingi 347,151,286 wakati katika kipindi cha Julai hadi Novemba kivuko
kilifanikiwa kukusanya shilingi 429,078,050 na kufanya jumla hiyo hapo
juu"ilisema sehemu ya taarifa ya Magreth.
kwa mujibu wa meneja huyo kunachangamoto ya mafuriko na uharibifu
mkubwa wa miundombinu,magari kugonga kivuko na kutumbukia majini,majani na
nyavu kujisokota kwenye mfumo wa usukani wa kivuko na mchanga kujaa mtoni
kunakosababisha kina kupungua.
Kwa upande wao wajumbe wa bodi ya kivuko hicho akiwemo mbunge wa
jimbo la Ulanga magharibi Dk Haji Mponda walimtaka wakala wa ufundi na umeme
Temesa mkoa wa Morogoro kuharakisha ujenzi wa vibanda vya kujikinga na mvua na
jua kivukoni hapo.
Aidha walikitaka kivuuko hicho kuongeza pato lake ili kiweze
kumudu kugharimia changamoto zinazojitokeza na kukifanya kuwa na tija katika
utendaji wake.
Wazo hilo liliungwa mkono na mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni
mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala akionyesha masikitiko yake ya jinsi
ambavyo mawazo ya bodi hayatekelezeki na kukatisha tamaa bodi hiyo kwa ushauri
wake.
No comments:
Post a Comment