Saturday, December 20, 2014

GERALD akiri kuwa Man U ilikuwa bora



Kocha wa Liverpool Steven Gerald

NAHODHA wa kilabu ya Liverpool Steven Gerrard amekiri kuwa Manchester United ilikuwa bora ikilinganishwa na Liverpool wakati timu hizo mbili zilipochuana wikendi iliopita lakini anasema kuwa hatokubali kushindwa na Arsenal wikendi hii.
Man United iliicharaza Liverpool 3-1 katika mechi hiyo.
Lakini Gerrard anaamini kwamba motisha uliopatikana katika timu hiyo baada ya kuishinda kilabu ya Bournemouth 3-1 katika mechi ya Kombe la Ligi na hivyobasi kuingia katika semi fainali na chelsea inaiweka timu hiyo katika nafasi nzuri dhidi ya Arsenal siku ya jumapili.
''Tofauti ya siku ya jumatano ikilinganishwa na siku ya jumapili ni kwamba tulifanya makosa makubwa katika uwanja wa Old Trafford na tukaadhibiwa na wachezaji wa kimataifa'',alisema Gerrard.
''Dhidi ya Bournemouth tulipunguza makosa hayo na kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri sana pengine tunaweza kusema tulikaribia viwango vya msimu uliopita''.aliongezea.

No comments:

Post a Comment