Saturday, December 20, 2014

JAMHURI ya Afrika ya kati kukumbwa na baa la njaa



Wananchi wa Afrika ya kati wakipatiwa chakula

SHIRIKA  la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea baa la njaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusema kuwa, watakaoathirika zaidi ni watoto wadogo.
Shirika hilo limesema, kutokana na ukosefu wa amani na usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na kutokuweko fedha za kutosha kwenye akiba yake, kuna uwezekano mkubwa shirika hilo likashindwa kuwasaidia watoto wa nchi hiyo iwapo baa la njaa litazuka.
 Taarifa ya shirika hilo la UN imesema, kwa sasa kuna takriban watoto milioni 2 huko CAR wanaohitaji misaada ya dharura ya dawa na chakula na kwamba hali inaweza kuwa mbaya iwapo shirika hilo halitapata fedha za kutosha kwa wakati ufaao.
Huku hayo yakijiri, shirika jingine la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema, Jamhuri ya Afrika ya Kati itashindwa kujidhaminia mahitaji ya chakula katika miezi michache ijayo. WFP limesema kwa sasa zaidi ya watu milioni 1.5 wanahitaji misaada ya chakula na kwamba idadi hiyo itaongezeka katika siku zijazo.

No comments:

Post a Comment