Saturday, December 20, 2014

RAIS Uhuru Kenyata aidhinsha sheria ya usalama



Rais wa Kenya Uhuru Kenyata

RAIS  wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.
Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.






No comments:

Post a Comment