Saturday, December 20, 2014

MGOMBEA wa Chadema aanguka na kufariki




Viongozi wakuu wa Chadema
MTU mmoja Rajabu Kikambako aliyekuwa mgombea kupitia Chadema nafasi ya ujumbe wa serikali ya kijiji cha Viwanja 60 kata ya Kamwene wilayani Kilombero ameanguka na kufariki dunia akiwa foleni kusubiri kupiga kura kituoni kwake.

Kwa niaba ya mwenyekiti wa Chadema wilayani humo katibu mwenezi wa chama hicho Anthon Kamonalelo Marehemu alifariki Desemba 14 na kuzikwa Desemba 15 baada ya kuanguka kwa kusimama muda mrefu kwenye foleni kulikosababishwa kasoro za zoezi hilo.
.
Mbali na hilo vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wanachi-Ukawa vimenyakua zaidi ya vijiji 57 kati ya 110,witongoji 225 kati 495 na Mitaa 29 mjini Ifakara kati ya 33 wilayani humo.

Katika ufafanuzi wake kati ya vijiji 57 ushindi kupitia Ukawa Chadema kimenyakua vijiji 45 chama cha wanachi CUF 32 wakati kati ya vitongoji 225 Chadema imevinasa 192,CUF 32 wakati chama cha NCCR-Mageuzi kikiambulia kitongoji kimoja.

Pia aliitaja Kata ya Utengule yenye vijiji 3 na vitongoji 12 wanavyotaraji kuvinyakua kwa ushindi wa kimbunga kimbunga katika uchaguzi unaotaraji kurudiwa hapo Desemba 21nchini kote.

Alisema baada ya uchaguzi kukamilika chama cha Demokrasia na mendeleo Chadema kimeandaa tafrija kubwa kwa washidi wote kupitia Ukawa,kupata mafunzo ya nidhamu na utushi wa umma itakayokwenda sambamba na safafari ya mafunzo katika moja ya vikao vya bunge mjini Dodoma.
“kwanza chama kimewapa tahadhari kama kunamtua anakuja kwa tama basi atangaze kujitoa kabla hajaaibika kwani wao ni wahudumu wa wananchi na hivyo wanapaswa kuwawezesha wananchi kwa kuhuduma bure…hakuna hata mtoto atakae andikishwa kwa fedha,vibali vyote vya huduma bure”aliongeza Kamonalelo





No comments:

Post a Comment