![]() |
Ajuza Priscilla akiwa darasani |
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya 'Leaders Vision Preparatory School' miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
No comments:
Post a Comment