Friday, January 16, 2015

MKUU wa wilaya ya Mvomero awataka wabakaji kujisalimisha


Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka
MKUU wa wilaya ya Mvomero Anthon Mtaka amewataka wabakaji na wazazi wanaowakatisha masomo watoto kike chini ya miaka 18 kutafuta mapori ya kukimbilia.
.

Rai hiyo aliitoa Mlali wakati akifungua mafunzo ya siku tatu juu ya uwajibikaji wa serikali  na wananchi katika utekelezaji wa sera ya elimu yaliyoandaliwa na asasi ya Kumbura Twiyapve group ikishirikiana na Foundation for civil society.

Alisema yeye binafsi hatakubaliana na suala la watoto kuendelea kuachishwa masomo kwa makusudi iwe kwa sababu yoyote wakati huu wa uongozi wake wilayani humo na kama kunamtu hakubaliani nae basi atafute pori la kukimbilia kuepusha shari.

Aliwataka watendaji,madiwani,walimu,watu wa usalama na wenye nia ya kuwasaidia watoto wa kike zikiwemo asasi kuwa na rejesta ya kuchunguza mienendo ya watoto hao na kutoa taarifa haraka kunakohusika

No comments:

Post a Comment