Friday, January 16, 2015
UTATA waibuka kati ya CCM na wafanyabiashara manispaa ya Morogoro
HOFU ya kuibuka vurugu baina ya wafanya biashara wenye vibanda eneo la Uwanja wa sabasaba na uongozi wa chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Morogoro.
Hofu hiyo inatokana na mahakama kuu kitengo cha ardhi nchini kwenye hukumu ya kesi namba 04/2014 ya 20/10/2014 kwa Jaji Hamisa Kalombola na kesi namba 199/2010 ya 27/11/2014 kwa Jaji Lameck Mlacha kuwathibitisha wafanyabiashara hao katika umiliki wa vibanda hivyo huku CCM nayo kuendelea kudai ni vibanda vyake.
Akizungumza katika ofisi za chama cha waandishi mkoa MOROPC msemaji wa wafanya biashara hao Robert Mluge alisema Mvurugano huo unaoweza kutokea kufuatia katibu wa chama hicho wilaya katika tangazo lake la 6/1/2015 kuwataka kuwasilisha mikataba na risiti za umilikaji huo 8/1/2015 ofisini kwake.
Katika baadhi ya majibu kwa waandishi Mluge alisema kwa mujibu wa hukumu hizo wafanya biashara hao hawapashwi kubughudhiwa nakuwa wamepewa uhuru wa kupangisha na kukodisha kwakua ni wajenzi wa vibanda hivyo vinavyo zunguka soko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment