POLISI katika nchi kadhaa barani Ulaya
wamewakamata washukiwa kadhaa wenye iktikadi kali za kidini katika misako
iliyofanywa usiku kucha.
Ripoti kutoka nchini Ufaransa zinasema kuwa washukiwa wanane wametiwa mbaroni, kuhusiana na mashambulio ya wiki iliyopita ambako watu kumi na saba waliuawa.
Afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo amesema kuwa washukiwa hao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na madai ya kuwasaidia washambuliaji kwa kuwabebea silaha au kuwapa usafiri .
No comments:
Post a Comment