Rais wa Niger |
WAISLAMU
duniani wakiendelea kulaani hatua ya kuvunjiwa tena heshima Mtume Mtukufu
Muhammad SAW na gazeti la vibonzo la Ufaransa
.
Niger imepiga marufuku
kusambazwa nakala za gazeti hilo nchini humo. Serikali ya Niamey pia imelaani
vikali hatua ya gazeti la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo
vinavyomkejeli Mtume Mtukufu SAW na kusema kwamba, hatua hiyo ni ya kichochezi,
mbaya na isiyokubalika kabisa na ndio sababu Rais wa Niger na serikali yake
wameamuru kupigwa marufuku kusambazwa na kuuzwa nakala za jarida hilo. Rais
Mahamadou Issoufou wa Niger ni miongoni mwa marais 6 wa Afrika walioshiriki
maandamano ya Paris ya kukumbuka wahanga wa mashambulizi yaliyolenga ofisi ya
gazeti hilo siku kadhaa zilizopita.
Wakati huo huo Waislamu duniani kote na
nchi mbalimbali wameendelea kulaani hatua hiyo ya kuvunjiwa heshima Mtume
Mtukufu SAW na jarida la Ufaransa. Maandamano ya kulaani hatua hiyo yamefanyika
katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu kama vile Kuwait ambako
waandamanaji walikusanyika mbele ya Ubalozi
No comments:
Post a Comment