CHAMA cha
soka cha Africa (CAf) kimetangaza kufanyika kwa vipimo vya ugonjwa wa ebola
katika michuno ya kombe la Mataifa ya Afrika.
Wachezaji viongozi na washabiki wote
watakaowasili katika nchi ya Guinea ya Ikweta watafanyiwa uchunguzi ya ugonjwa
huo.
Kulingana na taarifa za Caf timu ya kwanza
kuwasili nchi humo, Cape Verde walifanyiwa uchunguzi wa afya na itaendelea
kufanyika kwa wageni wote wataowasili.
Guinea ya Ikweta imekuwa mwenyeji wa michuano
hiyo baada ya Morocco waliokuwa wenyeji kujitoa kwa sababu za maambukizi ya
ugonjwa wa Ebola
No comments:
Post a Comment