Rais wa Iran kushoto akiwa na mgeni wake |
RAIS wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi amempokea katika Ikulu ya Saad
Abad Rais Nocolaus Maduro Moros wa Venezuela.
Rais Nicolaus Maduro jana usiku aliwasili
Tehran kwa minajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Rais Hassan Rouhani alimkaribisha rasmi katika
ikulu ya Saad Abad hapa Tehran Rais Nicolaus Maduro wa Venezuela baada ya
kupigwa nyimbo za taifa za nchi mbili na marais hao kukagua gwaride
maalumu.
Tayari viongozi wa Iran na Venezuela wameanza
mazungumzo rasmi. Ajenda kuu ya mazungumzo hayo kati ya Caracas na Tehran
imetajwa kuwa ni kuhusu kuimarishwa uhusiano na ushirikiano wa pande mbili,
kieneo na kimataifa. Rais wa Venezuela ameanza ziara zake za kimataifa tangu
Jumapili wiki iliyopita kwa kuitembelea China na nchi kadhaa wanachama wa
Jumuiya.
No comments:
Post a Comment