Saturday, February 14, 2015

MRADI wa Mkaa Endelevu kuendelea wilayani Kilosa



Wanakikundi wa mkaa Endelevu wakiwa kazini

KONGAMANO la mkaa Endelevu limemalizika na kukubaliana kuwa mradi wa mkaa Endelevu uendelee wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.


Akifunga kongamano hilo mwishoni mwa wiki, mjini Kilosa, Mkuu wa wilaya ya Kilosa Eliasi Tarimo ambaye alikuwa mwenyekiti wa kongamano alihitimisha kwa kuruhusu kuendelea kwa mradi huo kwa masharti ya kuchagua miti inayofaa kwa mkaa(selective)na si kukata miti yote (clear felling)kwani  ni hatari kwa uahi na usalama wa miti.

Mradi wa mkaa Endelevu unafanyika wilayani Kilosa ukiwa ni majaribio , unaendeshwa na Taasisi ya uhifadhi wa Misitu(TFCG),  kwa kushirikia na Mjumita wakifadhiliwa na serikali ya Uswisi.

Wataalamu bobezi wa misitu toka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Morogoro wakiongozwa na mtaalamu Nguli masuala ya Misitu Profesa Romanus Ishengoma wasilisha mada mbalimbali juu ya faida na madhara ya ukataji miti sanjari na urasimishaji wa biashara ya mkaa nchini.

No comments:

Post a Comment