Saturday, February 14, 2015

SAUDIA yatuhumiwa kuchochea mgogoro wa Yemen



Wananchi wa Yeman wakiwa katika maandamano
SHIRIKA la habari la Associated Press la nchini Marekani limetangaza kuwa, utawala wa Saudia unayachochea na kuyapatia silaha makabila yaishio katika mipaka ya kusini mwa Yemen kwa lengo la kuanzisha vita dhidi ya Harakati ya Answarullah ya nchi hiyo.

 Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa shirika hilo, jeshi la Misri nalo linajiandaa kuingia kijeshi nchini Yemen kwa kisingizio cha kulinda lango la Babul-Mandab. Kwa mujibu wa AP, hali ya hatari imetanda nchini Yemen kufuatia hatua ya Wamagharibi kuwaondoa wanadiplomasia wake nchini humo siku ya Jumatano, na kusisitiza kuwa hivi sasa Riyadh inayapatia silaha na zana na kivita makabila yaishio katika maeneo ya kusini mwa Yemen.
Aidha AP imewanukuu viongozi wa ngazi za juu nchini Yemen ambao hawakutaka kutaja majina yao, wakieleza kuwepo njama za pamoja kati ya Saudia na Misri kwa lengo la kuanzisha mashambulizi kwa uungaji mkono wa Marekani dhidi ya Yemen. Imefafanua zaidi kwamba, Saudia imekuwa ikituma silaha kwa makabila ya mkoa wa Ma'rib katika kipindi chote cha mgogoro wa kisiasa nchini humo.



No comments:

Post a Comment