![]() |
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Prof John Nkomwa |
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa
kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.
Kauli
hiyo ameitoa jana wakati akikabidhi leseni kwa radio Jembe FM.
Alisema
matumizi yasiyo sahihi yatasababisha mamlaka hiyo kunyang’anya leseni walioitoa
kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Alisema
pamoja na haja ya kushiriki katika ushindani, kituo hicho kipya kinatakiwa
kufuata masharti ya utangazaji ambayo yamo katika leseni waliyoiomba.
Alisema
radio hiyo ya Mwanza inaongeza ushindani katika eneo hilo katika jumla ya radio
FM 12 zinazosikika mjini humo, radio za kitaifa saba, za kikanda 11 na radio ya
jamii 1.
Aliwataka
kuwa waangalifu na kufuata kanuni za kitaalamua kufanyakazi wanasotahili za
kuelimisha na kuburudisha.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba wameanzisha
radio hiyo kwa lengo la zaidi ya kuburudisha na kuelimisha bali kusaidia vijana
kushika hatamu na kujitengenezea uwezo wa ajira.
Alisema
kwamba ili kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kitaaluma wameajiri watu ambao
wamesomea kazi husika ili kuhakikisha kwamba hawaendi kinyume na leseni yao.
Alisema
kwamba wanaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kujaza mapengo ambayo yapo katika
urushaji wa matangazo kwa sasa ili kuhudumia mji wa Mwanza ambao unakua kwa
kasi kwa sasa.
No comments:
Post a Comment