![]() |
Mheshimiwa Abdul Azizi Abood akiongea na wananchi |
MBUNGE wa jimbo la Morogoro AbdulAziz Abood ameonyesha hofu ya
machafuko katika uchaguzi ujao na kuziangukia Taasisi za dini mkoani humo
akizitaka kuimarisha maombi ya amani na utulivu ili tuvuke salama na kuendeleza
maisha.
Akihutubia kwenye kongamano la kuchangia
vifaa vya kanisa la Tanzania Assemblies o God viwandani mjini humo,Abood
aliwashauri waumini na viongozi wa dini vijembe na fitina kuwaachia wanasiasa
majukwaani.
“jamani vurugu tuisikie kwa wenzetu
tu katika nchi jiarani lakini janga hilo lisitukute,wanaoumia na kufa kama
nzige waliopulizwa dawa ni wanawake na watoto ambao ni warithi wa Taifa hili
baadae…jamani kwenye vita hakuna kula,kusali wala kukaa sehemu mkacheka kila mtu
ni adui yako”alisisitiza Abood.
Mbali na salamu hizo kwa taasisi za
dini,mbunge huyo amewataka wanaolitaka jimbo hilo kujitokeza kushindana
nae na kuvisihi vyama vya siasa kuwaandaa wagombea wao kisikolojia ili
waendeshe kapeni za kitaaluma pasipo kushawishika kufanya vurugu ambazo hatima
yake ni machafuko.
“nimebakiza wastani wa miezi mitatu
kumaliza ngwe yangu kwa mujibu wa katiba niliyoapa pale Dodoma na mimi nirudi
tena kuwaomba ridhaa nyingine ya kuwatumikia…nimzisikia nia na wengine
wanajinadi kuwa sinta rudi,leo nawaanbieni kuwa kwa mapenzi yake mungu nitarudi
tena”alifafanua.
Alitaja baadhi ya mambo makubwa
yaliyokuwa yakimuumiza kichwa na kukosa usingizi kabla hajaingia katika nafasi
hiyo kuwa ni pamoja kuziba mianya ya wizi wa fedha za umma katika halamashuri
ya manispaa,kuboresha huduma ikiwemo muindombinu kama barabara,maji,majengo na
kuwainua walalahoi kwa mitaji na maeneo ya kufanyia kazi.
Awali akimkaribisha kuzungumza na
waumini wa kanisa hilo,Mchungaji kiongozi Sauli Magawa aliemuunga mkono mbunge
huyo kwa kutangaza kurejea tena kwenye nafasi hiyo alisema kanisa hilo lenye
madhumuni ya kukomesha uovu kwa jamii,kuelimisha na kukemea maadili
linakabiliwa na upungufu wa vifaa mbalimbali zikiwemo spika,visemeo
visivyounganishwa na waya,kinanda na busta.
“vyote nilivyokutajia vinathamani ya
shilingi Mil 3,500,000 na tunaimani kuwa Mungu atatutangulia na kuvipata
kupitia wadau wa maendeleo ukiwemo wewe…umewasikia waumi wanavyokusihi kuwania
tena tunakuongeza nguvu ya kushawishika ufanye hivyo”alifafanua Magawa.
Hata hivyo Abood alichangia shilingi
500,000 na kuwasihi kutosita kumwalika hata kama hatakuwa ameshinda katika
uchaguzi ujao akidai hiyo ni dhamira yake tangu hajafikiria kuwania nafasi
hiyo.
No comments:
Post a Comment