Mheshimiwa Edward Lowasa akionesha fomu ya wadhamini mkoani Morogoro |
VIONGOZI
wakongwe wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Morogoro,wamekerwa
na tuhuma mbalimbali zinazoshushiwa chama Tawala.
Wakizungumza kwenye makabidhiano ya
fomu za udhamini ofisi ya CCM mkoa,wakongwe hao Dk.Juma Ngasongwa,Kanal Isack
Mwisongo,mwenyekiti wa wenyeviti wa ccm Mgana Msindai na Mwenyekiti ccm
wilayani Kilosa Nasoro Udulele kwa nyakati tofauti walionyesha kukerwa na
tuhuma pia dhamira ya jina la Edward Lowassa kukatwa kwenye vikao vya chama
njini Dodoma.
“hapa katikati uongozi wa chama
umeyumba na kupoteza mwelekeo,kila mtu ndani ya chama amegeuka kiongozi wa
kusema na kuamua atakavyo…mara tunaitana mizigo,wachafu hii yote ni kutokana na
kutokuwa na uongozi imara ambaye ni Lowassa”alisema Dk Ngasongwa.
Mbali na hilo Dk.Ngasongwa akinukuu
baadhi ya maneno ya watiania kumnyoshea kidole Lowasa,alihoji usafi wao ulipo
wakati tayari walikisaliti chama na kukimbilia upinzani na waliposhindwa huko
wakarudi wakiwa wamejikunyata kwa aibu.
“Lowasa ni dawa ya kukirejesha chama
na serikali kwenye matumaini ya kuwaongoza watanzania na kuwafikisha
wapatarajiapo,hakuwahi kuyumbishwa na vyama kama ilivyo kwa baadhi ya watia nia
ambao walikimbilia upinzani yalipowashinda wakarudi tena ccm…hatuwezi kuwaamini
hata kidogo”alifafanua zaidi.
Akitaja umahili wa Lowassa ndani ya
chama Mwenyekiti mstaafu Kanal.Mwisongo aliwataja Edward Lowasa,Ditopile
Mzuzuri na rais Jakaya Kikwete kuwa mwaka 1977 wakiwa vijana wenye shahada walikataa
kufanya kazi serikalini na kukimbilia chamani bila kujali ujira mdogo uliokuwa
huko.
“nikwa uwezo wenu mkakiwezesha chama
kufanya vema katika uongozi na chama kukua na kupendwa ndani na nje ya
nchi…kuna maneno kuwa ulikataliwa na Mwal.Julius Nyerere, mimi nakanusha
nikithibitisha kuwa nimekuwa nikishiriki vikao vyote vya chama hakuna hata
kikao kimoja ambacho Nyerere alisimama akamkataa”alisema Kanal Mwisongo.
No comments:
Post a Comment