Mashamba ya miwa kijiji cha Msolwa Ujamaa Kilombero |
CHAMA cha wakulima wa nje wa kilichopo kijiji cha Msolwa ujamaa(MUCGA) wilayani Kilombero, mkoa
wa Morogoro kinataraji kukusanya zaidi
shilingi 543,640,000 na kutumia shilingi 509,290,000 katika kipindi cha mwaka
2015/2016.
Pato hilo linatokana na chama hicho
kilichoanzishwa mwaka 2008 chenye wakulima wanachama 1,152 wenye ekari 5,210
kutaraji kuvuna zaidi ya tani 51,000 za miwa kisha kusindikwa na kutengenezwa
bidhaa ikiwemo sukari.
Mwenyekiti wa Mucga Sebastian
Sangilindege alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkuu na kubainisha
kuwa mafanikio hayo yamekiwezesha chama hicho kuaminika na taasisi za fedha
ikiwemo Benki ya CRDB na kuwakopesha shilingi Mil.520 zitkazo kwenda kw
wanachama 100.
"tunaendesha kazi zetu vizuri
na matunda yake ni zaidi wakulima 100 walio katika mashamba ya pamoja(block
farm) watapata mikopo ya jumla ya shilingi mil.520 kwa ajili ya kuendeleza
mashamba yao ya miwa"alifafanua Sangilindege.
Kwa mujibu wa mwenyekiti
Sangilindege baadhi ya vikundio vitakavyonufaika na fedha hizo kutoka CRDB ni
pamoja na Kumekucha,Mdokonyole,Usawa,Ushindi,MU1,MU5,MU11,MU17 na MU18.
Alitaja mafanikio mengine kuwa ni
chama kujiimarisha kwa kununua vitendeakazi ikiwemo mashine ya kupakilia
miwa,kuongeza mavuno hadi tani 55,000 toka kiwango walichopangiwa na kiwanda
cha sukari na kurekebisha miundombinu mashambani hasa sehemu korofi.
Aidha chama kimepunguza baadhi za
gharama zikiwemo za wakandarasi katika huduma za ukataji,upakiaji na
usafirishaji ni za chini ukilinganisha na vyama vingine vya wakulima wa miwa
katika bonde la Kilombero pia wamejitahidi kuwapatia pembejeo kwa gharama
nafuu.
"na katika msimu huu tunataraji
kujenga ofisi ya chama na utaratibu wa ujenzi upo tayari baada ya kupata hati
ya kimila,tunataraji mwezi Septemba ujenzi utaanza kwani tumetenga shilingi mil
40"alisema
No comments:
Post a Comment