UHABA wa fedha kwa Taasisi zisizo za kiserikali
zinazojishughulisha na Utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika Fukwe za Bahari
ya Hindi ni moja ya mambo yanayochangia uharibifu wa mazingira katika Fukwe
hizo.
Hayo yamebainishwa
leo na Muikolojia na kiongozi wa Taasisi inayojihusisha na uhifadhi wa mazingira Ferry jijini Dar es salaam Bwana
Mohamed Muhidini katika mahojiano maalum na kipindi cha Dira ya Mazingira wakati akielezea mikakati yao ya kutunza na kuhifadhi mikoko katika Fukwe za Bahari ya Hindi.
Amesema kuwa
, serikali inapaswa kushirikiana kikamilifu na Taasisi na Asasi mbalimbali za
Mazingira baharini, ikiwa ni pamoja na kuziwezesha kifedha na rasimali watu ili
kufikia malengo.
No comments:
Post a Comment