![]() |
Askofu Josephat Gwajima |
JESHI
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya
kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam.
Askofu Gwajima alifika kituo kikuu
cha Polisi saa nane na dakika kumi na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara
baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri
kufika kwake.
Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima
ni pamoja na kumkashfu na kumtukana hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo
Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Taratibu za mahojiano zimekwishaanza
kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa
na ndugu yake wa karibu, rafiki yake anayemwamini au wakili wake.
Kama ilivyo kawaida utakusanywa
ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio
hilo lilivyotokea na athari zake.
Baada ya hapo hatua nyingine za
kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya
kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika
upelelezi wa shauri hili, ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila
atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri
hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa katika jamii.
Mbona viongozi wengine wa kidini wakiongea maneno yenye uchochezi hawahojiwi?
ReplyDelete