Saturday, May 9, 2015

CHANJO dhidi ya malaria yaonesha dalili nzuri nchini Kenya


Rais wa Kenya Uhuru Kenyata
MAJARIBIO  ya chanjo dhidi ya malaria nchini Kenya yameonesha dalili nzuri ya mafanikio.

Wanasayansi watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford Uingereza wamesajili asili mia 67% ya mafanikio katika majaribio ya chanjo hiyo kwa wakenya 121.
Utafiti huo ni wa pili wa haiba yake katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Majaribio ya chanjo nyengine tofauti pia yameonesha mafanikio katika kuwakinga watoto wachanga.
Takwimu zinaonesha kuwa watoto 1,300 wanakufa kila siku chini ya jangwa la Sahara kutokana na ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa visa milioni 198 vya malaria viliripotiwa mwaka wa 2013 huku takriban watoto 584,000 wakipoteza maisha yao.
Ajabu ni kuwa hakujakuwa na mafanikio makubwa kuhusu mbinu za kupambana na kirusi kinachosababisha malaria.

No comments:

Post a Comment