Mbunge wa Morogoro mjini Abdul Aziz Mohamed Abood |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na
maafisa Afya kata zote 29 ofisi ya Afya Manispaa, Afisa afya mkoa Carle Lyimo
na Afisa afya Manispaa Gabriel Malisa walisema zoezi hilo linaloanza Mei 11
linalenga kuuepusha mji huo na magonjwa ya milipuko.
“kwenye hili tuache siasa
tukizingatia kanuni zetu za utumishi yani hakuana kilicho na thamani zaidi ya
uhai wa mtu,ikumbukwe kuwa kipindi hiki nicha masika,kina magonjwa hatari
yakiwemo ya milipuko sasa lazima tufanye kazi kabla ya athari”alisema Lyimo.
Aliongeza zoezi hilo
litakaloendeshwa kisayansi litaanza Mei 11 kwa kutambua matatizo yaliyo kwenye
nyumba na kujaza fomu namba moja sambamba na kupewa maagizo yatakayotakiwa
kutekelezwa ndani ya siku tatu.
Kuhusu wajasiliamali wakiwemo mama
na baba lishe,wafanya biashara ndogondogo aliwataka kuzingatia sheria na
taratibu za afya kwa kufanya shuguli zao huku akisisitia hakuana atakae
ruhusiwa kupanga chini bidhaa.
Afsa huyo alisema baada ya zoezi na
muda huo maafisa afya hao watapita tena kuhakiki kama maelekezo yametekelezeka
na kupewa alama A-D ambazo zitatumika kuwaburuza mahakamani.
Kwa upande wake Malisa aliwataka
watu wote waliotelekeza viwanja,magofu ya majengo,waliolima mjini na kupanda
mazao kinyume na sheria za mipango miji kuanza kuyafanyia usafi maeneo yao
kabla hatua za kisheria hazijawafikia.
“kunatabia ya watu kudharau
wakidhani kuwa hii ni nguvu ya soda pekee, mimi nawasihi kuepusha shari kabla
haijawakuta maana usafihuu hautakuwa wa muda mfupi kwani tunakusudia kuitumia
sheria yetu ya usafi kikamilifu” alisema Malisa
Hivi karibuni manispaa hiyo
ilipitisha sheria kali ya faini ya shilingi 50,000 kwa atakae bainika kufanya
uchafuzi wa mazingira katika mji huo ikiwa ni hatua moja wapo ya kuifanya
manispaa hiyo kuwa Jiji.
No comments:
Post a Comment